bayyinaat

Published time: 21 ,September ,2018      16:08:48
News ID: 337

بسم الله الرحمن الرحیم

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema mwenye kurehemu


1 KUSHUKA BALAA NA MAAFA:

Hakika dhambi yoyote, ni sababu ya kushuka balaa na mafa kwa mtu binafsi na hata jamii nzima, pia imenukuliwa ya kwamba, kila itokeapo dhambi mpya katika jamii, ndivyo maafa mapya na maangamio mabaya yaibukavyo, maradhi mapya, kama vile vifo vya haraka, hususan kwa vijana ambao ni rasilimali ya jamii, ongezeko kubwa la maradhi ya kiroho na kisaikolojia na kadhalika… na hiyo hutokana na aina ya athari ya madhambi mapya yatokeayo katika jamii.

Imam Sadiq (a.s) amesema:

"تَعَوَّذُوا بِاللهِ مِنْ سَطَوَاتِ اللّهِ بِاللَّیْلِ وَالنَّهَارِ قَالَ قُلْتُ لَهُ وَمَا سَطَوَاتُ اللّهِ قَالَ الْاَخْذُ عَلَی الْمَعَاصِی".

"Kimbilieni kwa Mwenyezi Mungu usiku na mchana kwa kuomba ushindi, akaulizwa: ni ushindi gani huo: akasema: Adhabu na mateso ya maasi”.

2 KUBDILIKA NEEMA ZA MUNGU:

Katika kitabu cha Mwenyezi Mungu ni kwamba, imeelezwa kuwa moja ya athari ya madhambi ni kuondokewa na neema za Mwenyezi Mungu, aidha katika surat al- Anfaal tunasoma kwamba:

"ذَلِكَ بِأَنَّ اللَّهَ لَمْ يكُ مُغَيرًا نِعْمَةً أَنْعَمَهَا عَلَى قَوْمٍ حَتَّى يغَيرُوا مَا بِأَنْفُسِهِمْ وَأَنَّ اللَّهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ".

"Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu habadilishi kabisa neema alizo waneemesha watu, mpaka wao wabadilishe yaliyomo ndani ya nafsi zao. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua”.

Katika hadithi mbalimbali, ziko riwaya tafauti zikielezea aina na sababu za kuondokewa na neema kama vile: Dhulma na dhambi, vilevile kurudi kutoka kwenye dhambi ya kuelekea njia ya haki ni sababu ya kuzidi kwa neema mbalimbali za Mwenyezi Mungu mtukufu.

Madhambi na dhulma ni mambo ambayo humnyima mwanadamu kupata ladha ya huruma ya Mwenyezi Mungu, pia imepokelewa katika hotuba ya Imam imeashiria mambo hayo, na katika Dua Kumail pia tunasoma:

"اَللَّهُمَّ اغْفِرْ لِیِ الذُّنُوبَ الَّتِی تُغَیِّرُ النِّعَمْ".

"Mola wangu nisamehe madhambi ambayo huondosha neema zako kwangu”.

Katika dunia hii ipo kanuni na sheria za kielimu ambazo kwamba zinakubaliana na hili, ikiwa kundi katika jamii litakithiri kutenda maovu ambayo huweza kuleta nakama kwenye jamii hiyo, hakika balaa hiyo huwashamili walio salama na wasio salama pia.

Katika barua ya Imam huyo mtukufu (a.s) kwa Malik Ashtar tunasoma:

"لَیْسَ شَی ءٌ اُدْعَی اِلَی تَغْیِیرِ نِعْمَةِ اللّهِ وَتَعْجِیلِ نِقْمَتِهِ مِنْ اِقَامَةٍ عَلَی ظُلْم".

"Hapana kitu kipelekeacho kubadilisha neema za Mwenyezi Mungu na kuharakisha nakama yake kuliko kusimamia dhulma”.

3 UHARIBIFU KATIKA JAMII:

Bila shaka, jambo lolote la ukiukaji wa kanuni lipatikanalo katika jamii na kwa njia hiyo likapelekea kuleta athari kwa mwanadamu, hakika husababisha aina fulani ya uharibifu katika nidhamu ya kijamii. Dhambi yoyote na kitendo kiovu na uvunjaji wa kanuni, ni mfano wa chakula kisichokuwa salama na chenye sumu ambacho huharibu mfumo mzima wa mwili wa mwanadamu, tutake tusitake bila shaka kitaleta athari mbaya mwilini, na mwanadamu huyo hupatwa na udhaifu mkubwa mno. Qur’ani tukufu inasema:

" ظَهَرَ الْفَسَادُ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ بِمَا كَسَبَتْ أَيدِي النَّاسِ لِيذِيقَهُمْ بَعْضَ الَّذِي عَمِلُوا لَعَلَّهُمْ يرْجِعُونَ ".

"Ufisadi umedhihiri bara na baharini kwa iliyo yafanya mikono ya watu, ili Mwenyezi Mungu awaonyeshe baadhi ya waliyo yatenda. Huenda wakarejea kwa kutubu”.[1]

Kwa kifupi ni kwamba, matatizo mengi ya jamii yetu husababishwa na dhambi zetu na maovu yetu ambayo miaka mingi tumekuwa tukiwahamasisha vijana wetu kutumia mbinu za maadui wenye lengo la kuharibu jamii zetu.

Ni wajibu wa walezi na viongozi wa dini kutumia njia sahihi za kuwaongoza vijana kuepuka silaha za adui hao, ambazo huwaingiza katika maasi na madhambi, kwanini wanawake wamekuwa ni wachache wa kujistiri, mahusiano yasiyo ya kisheria katika ya kijana wa kike na kiume pia ni moja ya mambo yanayoharibu jamii, ambayo huibuka mahusiano hayo kwa njia ya simu, intaneti pamoja na mitandao ya kijamii na kadhalika… ambapo Mwenyezi Mungu amekwisha amrisha nidhamu hii ya Kiislamu kuwa ni lazima ilindwe. Vile vile ziko riwaya mbalimbali kutoka kwa Maimamu watakatifu wameeleza kuwa; madhambi ni sababu ya jamii kutawaliwa na watu waovu na madhalimu.

Imam Baqir (a.s) anasema:

«وَجَدْنا فِی کِتابِ رَسُولِ اللَّهِ9 اِذا ظَهَرَ الزِّنا مِنْ بَعْدِی کَثُرَ مَوْتُ الْفَجْاَةِ وَاِذا طُفِّفَ الْمِکْیالُ وَالْمِیزانُ اَخَذَهُمُ اللَّهُ بِالسِّنِینَ وَالنَّقْصِ وَاِذا مَنَعُوا الزَّکاةَ مَنَعَتِ الْاَرْضُ بَرَکَتَها مِنَ الزَّرْعِ وَالثِّمارِ وَالْمَعادِنِ کُلَّها وَاِذا جارُوا فِی الْاَحْکامِ تَعاوَنُوا عَلَی الظُّلْمِ وَالْعُدْوانِ وَاِذا نَقَضُوا الْعَهْدَ سَلَّطَ اللَّهُ عَلَیْهِمْ عَدُوَّهُمْ وَاِذا قَطَّعُو الْاَرْحامَ جُعِلَتِ الْاَمْوالُ فِی اَیْدِی الْاَشْرَارِ وَاِذا لَمْ یَاْمُرُوا بِالْمَعْرُوفِ وَلَمْ یَنْهَوْا عَنِ الْمُنْکَرِ وَلَمْ یَتَّبِعُوا الْاَخْیارَ مِنْ اَهْلِ بَیْتِی سَلَّطَ اللَّهُ عَلَیْهِمْ شِرارَهُمْ فَیَدْعُوا خِیارُهُمْ فَلا یُسْتَجابُ لَهُمْ؛

"Tumekuta katika maandishi ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kwamba; Itakapodhihiri zinaa baada yangu basi yatakithiri mauti ya ghafla, na itakapopunjwa kilo na mizani Mwenyezi Mungu atawaletea ukame na upungufu wa riziki, na watakapo zuia kutoa zaka ardhi itazuia baraka zake za mimea na matunda na madini yote, na watakapokiuka hukumu watakuwa wamezaiana katika dhulma na uadui, na watakapo kwenda kinyume na ahadi Mwenyezi Mungu huwaletea adui yao kuwatawala, na watakapovunja undugu basi zitawekwa mali katika mikono ya watu waovu, na endapo hawatoamrisha mema na kukemea mabaya na hawakufuata wema katika watu nyumbani kwangu Mwenyezi Mungu huwaletea wabaya zaidi na wakati huo wataomba wema lakini hawatajibiwa”.

----------------------



[1] Al- Rum/ 41.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: