bayyinaat

Published time: 19 ,September ,2018      10:36:55
“Na tulimtuma Lut', alipo waambia watu wake: Je, mnafanya uchafu ambao hajakutangulieni yeyote kwa uchafu huo katika viumbe vyote!. Hivyo nyinyi mnawaingilia wanaume kwa matamanio mkawacha wanawake? Kumbe nyinyi ni watu wafujaji!”
News ID: 316


Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema mwenye kurehemu


KULAWITI NI UCHAFU MBAYA MNO

Kutoka kwa Imam Ridhaa (a.s): Ogopeni zinaa na kulawiti, na hakika kulawiti ni kitendo kibaya mno kuliko zinaa, na viwili hivyo humsababishia mwenyewe maradhi sabini na mbili duniani na akhera.[1]

Aidha Mwenyezi Mungu amekwisha abiri kuwa kulawiti ni uchafu mbaya kama alivyo abiri zinaa aliposema katika kitabu chake kitukufu:

" وَلُوطًا إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ أَتَأْتُونَ الْفَاحِشَةَ مَا سَبَقَكُمْ بِهَا مِنْ أَحَدٍ مِنَ الْعَالَمِينَ. إِنَّكُمْ لَتَأْتُونَ الرِّجَالَ شَهْوَةً مِنْ دُونِ النِّسَاءِ بَلْ أَنْتُمْ قَوْمٌ مُسْرِفُونَ".

"Na tulimtuma Lut', alipo waambia watu wake: Je, mnafanya uchafu ambao hajakutangulieni yeyote kwa uchafu huo katika viumbe vyote!. Hivyo nyinyi mnawaingilia wanaume kwa matamanio mkawacha wanawake? Kumbe nyinyi ni watu wafujaji!”.[2]

Ni uharibifu mkubwa ulioje wa kuweka mbegu – ambazo ni mzizi wa kudumisha uwepo wa jamii za binadamu na kizazi na ambazo ni wajibu kuweka ndani ya kifuko cha mwanamke – katika mahali ambapo Mwenyezi Mungu hakupaumbia.

Na ili kukomesha wengine kukaribia amali hii chafu inayopingana na uwepo wa mwanadmu, Mwenyezi Mungu mara kwa mara hukariri kauli na ukumbusho wa kisa cha Lut na namna alivyowaadhibu katika sura zifuatazo: Al- A’raaf, Hud, Al- Naml, Al- A’nkabut, al- Qamar na al- Najm.

JICHO LA MATAMANIO KWA KIJANA WA KIUME NI HARAMU

1. Imeharamishwa kumtazama mvulana kwa jicho la matamanio. Na tumekwisha bainisha natija yake mbaya na ukali wa adhabu ya kumuangalia kwa upana zaidi katika pekuzi ya zinaa.

Imepokelewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w): Jiepusheni na watoto wa matajiri na watawala wasiopevuka, kwani fitina zao ni kali mno kuliko walipevuka.[3]

Hivyo lazima juu ya kila muislamu kuzinduka ukweli wa kuzinduka ili asitahiniwe kwa dhambi hii kubwa ndani ya maisha yake.

LIJAMU YA MOTO KWA BUSU LA MATAMANIO

2. Imeharamishwa kumbusu kijana kwa matamanio kama ilivyonukuliwa kutoka kwa Imam Sadiq (a.s) hadithi iliyotoka kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) akisema: "Yeyote atakayembusu kijana kwa matamanio Mwenyezi Mungu atamvuta siku ya kiama kwa lijamu ya moto wa jahannam”.[4]

Na imepokelewa kutoka kwa Imam Ridhaa (a.s): Na mwanaume atakapombusu kijana kwa matamanio watamlaani malaika wa mbingu na nchi na malaika wa rehema na ghadhabu, na Mwenyezi Mungu atamuandalia adhabu ya jahannam na mafakio yake ni mabaya.[5]

Na aidha kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) amesema: Yeyote atakayembusu mvulana kwa matamanio Mwenyezi Mungu atamuadhibu miaka elfu moja ndani ya moto.[6]

Na endapo itathibi ya kwamba mwanaume amembusu mvulana kwa kmtamani ni wajibu kuadhibiwa, na adhabu yake ni kuanzia bakora thalathini hadi tisini, na mpangiliaji wa amri hiyo hukabidhiwa Hakimu wa kisheria kulingana na masilahi ayaonayo yeye.

KULALA WANAUME WAWILI NA WANAWAKE WAWILI

3. Ni haramu wanaume wawili kuchangia kitanda kimoja na shuka moja ilihali wakiwa uchi, na hukumu yake ni mfano wa hukumu ya wanawake wawili na hapana tofauti kati ya ajinabi au ndugu wa damu.

Na imepokelewa katika baadhi ya riwaya ya kwamba ni wajibu kupewea adhabu, na adhabu zao ni bakora mia moja.

Na baadhi ya maulamaa wamekihesabu kitendo hiki kuwa ni katika madhambi makubwa, kwani kina adhabu ndani yake kwa kukitenda.

Kutoka kwa Mtume (s.a.w.w): Ala ala mujihimize na kijana wa kiume na kijana wa kike, watenganishwe kitandani wafikiapo miaka kumi.[7]

----------------------

Imekusanywa na:

Ndg: Juma. R. Kazingati.



[1] Fiq’hi al- Ridhaa (a.s), uk 277 – mlango; al- zinaa wa al- liwaat.

[2] surat al- A’raaf, Aya 80 81.

[3] Al- wasaail kitab al- Nikaar, juz 14, uk 257, mlango 21, hadithi 2.

[4] Al- wasaail, juz 14, uk 257, mlango; Tajriim muqaddimaat al- liwaat, hadithi 1.

[5] Fiq’hi al- Ridhaa (a.s), uk 278, mlango; al- zinaa wa al- liwaat.

[6] Al- mustadrak, juz 14, uk 351, mlango; Tajriim muqaddimaat al- liwaat, hadithi 4.

[7] Al- wasaail, juz 14, uk 267, mlango 29, hadithi 1, pamoja na kuwepo khitilafgu baina yake.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: